Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kufuatia mashambulizi ya Iran dhidi ya "Beersheba" Kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa na Israel kwa mabavu leo hii asubuhi (24-06-2025) na kulazimika kwa utawala huo ghasibu wa Kizayuni kuomba usitishaji vita, Rais Isaac Herzog wa Israel ametangaza kuwa, Tel Aviv imelipa gharama kubwa mno katika damu ya wakaazi (walowezi wa kizayuni) wa maeneo ya Israel (bali ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Israel) katika vita na Iran.
Katika hotuba yake akigusia kadhia ya wafungwa wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza amesisitiza kuwa, kuwarejesha mateka wa Kizayuni kutoka Gaza ni jukumu takatifu hadi watakaporejea wafungwa wote wakiwa hai au wamekufa, ushindi kamili katika vita hivyo haujapatikana.
Your Comment